Matendo 12: 5, ukisoma huu mstari wa tano utaona umuhimu wa kuombea kiongozi wa maono kama ambavyo kanisa lilimuombea Petro na akafunguliwa katika vifungo vyake.
KWANINI TUOMBE KWA JUHUDI KWA AJILI YA KIONGOZI?
Kwasababu kuna mambo mengi ambayo anakutana nayo ambayo hawezi kuyashinda peke yake lazima tuwe wengi tunayesimama naye, soma Kutoka 17:11-13 , ukisoma habari hii utaona jinsi ambavyo
Musa aliponyanyua mikono peke yake alichoka na alipochoka walishindwa vita, lakini Haruni na Huri walipomsaidia walishinda vita.
Elewa kuwa kazi ya kumuombea mchungaji kiongozi sio ya
watu fulani, ni yako wewe pia. Acha kuangalia watu wengine fanya wewe kama vile hakuna mtu mwingine. Jambo hili liwe sehemu ya maisha yako ya kila siku
No comments:
Post a Comment