Breaking News

Thursday, February 27, 2014

KUOMBEA TANZANIA

Soma  : 1Yohana 4:7 

Wapenzi na tupendane kwa kuwa pendo latoka kwa Mung na kila apendaye amezaliwa na Mungu naye anamjua Mungu.

A.  Tuombee Taifa letu la Tanzania mbele za Mungu, Watanzania wote wapewe pendo la Mungu katika  maisha yao waweze kupendana kama ndugu. Omba upendo wa Mungu uweze kufuta :-

  • Chuki

  • Ubaguzi wa kidini

  • Ubaguzi wa kisiasa

  • Ubaguzi wa kikabila

  • Ubaguzi wa rangi na tofauti za kijinsia

B.Tuwaombee Watanzania wote wamilikiwe na upendo wa Mungu katika imani zao, katika  elimu zao, biashara zao na tabaia zao za asili au tabia zao za kidini ,upendo upate kuwaongoza.

1Yohana 4:21 "Na amri hii tumepewa na yeye ya kwamba yeye ampendaye Mungu ampenda na ndugu yake". Tuombee watanzania wote wanaoamini katika dini mbalimbali zinazomkiri Mungu wapokee amri hii kuwa upendo wao kwa Mungu wauonyeshe kwa kuwapenda ndugu zao.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

UNAITUMIAJE NAFASI ULIYONAYO?

Kufanikiwa kwako katika maombi kunategemea unavyoitumia nafasi yako uliyonayo katika ulimwengu wa Roho. Jadili

Breaking News