Ukisoma kitabu cha mwanzo 39 na kuendelea utakutana na habari ya Yusuph mtu aliyempenda sana Mungu.Tuangalie kwa pamoja ule mstari wa tisa sura hii ya 39 ; utaona jinsi ambavyo hofu ya Mungu ndani ya moyo wa Yusufu alimfanya akatae kufanya dhambi maana walikuwa wawili tu kama si kuwa na hofu ya Mungu hakika angefanya dhambi na watu wasingejua chochote.
Katika kitabu cha Daniel 3: 3-17 hawa watu kwasababu ya kuwa na hofu ya Mungu walikubali kutupwa ndani ya tanuru kuliko kumkosea Mungu kwa kuabudu sanamu zisizo na uhai. Pia katika kitabu cha Ester 3:1-2 utaona Mordekai akikataa kumsujudia Hamani kwasababu haikuwa sawa kumsujudia mwanadamu.
Swali je, ni mara ngapi umekutana na changamoto katika maisha yako na ukaisujudia? Ukasahau kuwa neno linasema msujudie Mungu peke yake? Pia Paulo anasema ni kitu gani kitanitenga na upendo wa Mungu. Akaviorodhesha vitu vingi katika kitabu cha Warumi 8: 35 ; soma haya maandiko utaona hofu ya Mungu ndani ya Paulo ilivyokuwa kubwa.
Mpendwa uwe na hofu ya Mungu ili ujiepushe na dhambi za dunia hii.
MAOMBI.
Mungu achilia hofu yako ndani ya moyo wangu katika kukutumikia, 2Nyakati 19:7
Omba sawa na Zaburi 4: 4
Omba hofu ya Mungu ikuingie Matendo 19:7
Omba sawa na Efeso 6:5
No comments:
Post a Comment