Breaking News

Monday, March 3, 2014

ISHI MAISHA YA KUSAMEHE

Ni jambo la muhimu sana mbele za MUNGU kuwa na maisha ya kusamehe, maana neno linasema " Sisi je tutapataje kupona tusipo jali wokovu mkuu namna hii? Waebrania  2: 3.
Kusamehe huachilia wokovu katika maisha yetu, ndio maana asiyeweza kusamehe naye hatasamehewa na Mungu Mathayo 6: 15.

MAOMBI

  • Omba : Mungu nisamehe makosa yangu yote niliyokukosea kwa kuwazia, kuwatendea na kuwanenea vibaya wale wote walionikosea.
  • Omba : Mungu nisaidie niweze kusamehe saba mara sabini (Mathayo 18:21-22)
  • Omba : Mungu nisaidie kila nisimamapo kusali kwanza nisamehe walionikosea(Marko 11: 25)
  • Omba: Mungu nisaidie niweze kuchukuliana na kusamehe( wakolosai 3: 13)
  • Omba: Mungu nisamehe na roho ya uchungu inayosababishwa na kutokusamehe.
  • Omba : Mungu nisaidie kuwa mtu ninayesamehe ili majeraha ya ndani yasiwepo katika maisha yangu.
Omba kwa uaminifu maana MUNGU analojibu kwa ajili yako.
MUNGU AKUBARIKI

No comments:

Post a Comment

Featured Post

UNAITUMIAJE NAFASI ULIYONAYO?

Kufanikiwa kwako katika maombi kunategemea unavyoitumia nafasi yako uliyonayo katika ulimwengu wa Roho. Jadili

Breaking News